Programu ya Huduma za Usaidizi kwa Wateja wa Google (GSS) hukuruhusu kushiriki skrini ya kifaa chako cha Android na mhudumu wa kituo cha usaidizi kwa wateja wa Google ili upate usaidizi maalum. Ukiwa na GSS kwenye kifaa chako, mhudumu anaweza kukuomba ushiriki skrini yako na kukuongoza kupitia vidokezo kwenye skrini. Hivyo basi, tatizo lako litasuluhishwa haraka. Wakati unashiriki skrini yako, mhudumu hataweza kudhibiti kifaa chako lakini ataweza kuona skrini yako ili aweze kukupa maelekezo. Unaweza kusitisha au kukatiza kabisha kushiriki skrini yako wakati wowote.
Programu hii huwa imesakinishwa kwenye vifaa vya Pixel na Nexus vinavyotumia toleo la Android 7.1.1 au mapya zaidi; pia inaweza kusakinishwa kwenye vifaa vingi vinavyotumia toleo la Android 5.0 au mapya zaidi. Programu hii haiwezi kujianzisha yenyewe na hutumika tu wakati mhudumu wa kituo cha usaidizi kwa wateja wa Google anatuma mwaliko kwa mtumiaji kushiriki skrini yake.
Ilisasishwa tarehe
31 Okt 2022